• Breaking News

    Agribussiness Transformation, Poverty Wiper.

    Recent Posts

    Saturday 20 August 2016

    KILIMO CHA VITUNGUU - ZAO LA VITUNGUU KIBIASHARA




    Vitunguu ni zao ambalo limekuwa likilimwa kwa wingi sehemu nyingi duniani.Pamoja na wengi wakitegemea kilimo hichi kwa njia ya umwagiliaji wapo waliofanya kilimo hichi kwa kutegemea misimu mbali mbali ya mvua.Kwa hapa kwetu bado tunayo mazingira sahihi kabisa kwa shughuli hii.Ni vyenya biashara hii kwa kupata maelezo kidogo ya jinsi vinavyolimwa na soko lake lilivyo na ni kinanni wanaweza fanya kilimo hichi kibiashara.


    VITUNGUU

    Kiuhalisia kitunguu ni moja kati ya mazao yanayotumiwa karibu kila siku katika mlo wa familia nyingi inchini kwetu Tanzania na sehemu nyingine duniani.Mara nyingi vitunguu vimekuwa vikitumika katika maandalizi ya mboga nyingi hasa sehemu za mijini.

    MATUMIZI YA VITUNGUU

    Yapo matumizi mengi sana ambayo yanafanya vitunguu kuhitajika kibiashara.

    Matumizi hayo ni kama:
    • Kutumika katika kutengenezea kachumbari
    • Kama kiungo cha mboga,nyama na samaki,
    • Majani yake pia hutumika kama mboga pia,
    • Hutumika katika maandalizi ya supu.

    Matumizi haya ambayo yamekuwa yakiitajika katika mlo wa mchana au usiku wa watanzania unafanya kitunguu kuhitajika sana katika jamii ya kitanzania.

    MAHITAJI KATIKA KILIMO CHA VITUNGUU

    Ili zao la vitunguu liweze kuota na kustawi vyema yapo mambo mengi inabidi kuyafahamu.Mambo haya yakifahamika itachangia katika kupata mazao kadri ulivyokusudia.Mambo hayo ni:
    • Zao hili hustawi sehemu zisizokuwa na mvua nyingi sana,
    • Sehemu zenye baridi kiasi,
    • Sehemu zisizo na joto kali,
    • Zao hili hustawi sehemu zenye udongo wa rutuba ya kutosha,
    • Hustawi sehemu zenye udongo unaoruhusu mizizi kupenya kirahisi,
    • Zao hili hustawi kwenye udongo unao hifadhi unyevu.

    UPANDAJI WA KWENYE KITALU

    Kabla vitunguu havijapandwa kwenye bustani hupandwa kwenye vitalu.Sababu wakulima wengi hapa kwetu hupanda kwa msimu vitunguu hivi wengi hupendelea kupanda mbegu za vitunguu kwenye vitalu kuanzia mwezi wa tatu(3) mpaka wa tano(5) .Maranyingi kilimo hichi huanza pale mvua za masika zinapokwisha.Hali hii hufanya ukuaji wake kuwa katika kiangazi na baridi.

    Upandaji wa mbegu kwenye vitalu unaweza kuwa wa aina mbili:
    • Kupandwa kwa mstari,
    • Kupandwa kwa kutawanywa.

    Kama itapandwa kwa mstari basi umbali kati ya mstari na mstari iwe kati ya sentimeta 10 mpaka sentimeta 15.

    Mbegu hupandwa kwa kufunikwa na udongo pia na nyasi kavu au matandazo juu ya tuta husika.

    Mbegu ikishaota nyasi zilizofunikia hutolewa na baada ya hapo kichanja inabidi kijengwe kwa ajili ya kivuli cha kitalu husika.Kichanja hicho kitakuwa cha nyasi.

    Baada ya siku saba(7) mpaka kumi(10) mbegu zinakuwa zimeshaota.

    UPANDAJI WA MICHE KWENYE BUSTANI

    Wakati wa kupandikiza miche kwenye bustani unashauriwa kutokukata miche wala kupunguza majani.Na umbali kati ya mche na mche ni sentimeta 10 na umbali kati ya mstari na mstari ni sentimeta 30.

    MATUNZO YA BUSTANI YA VITUNGUU:
    Zao la vitunguuu huitaji maji ya kutosha katika kipindi cha ukuaji wa mmea hasa wakati wa kutunga tunguu,
    Sehemu sinazokosa mvua ni vyema umwagiliaji ufanyike,
    Ili vitunguu vikomae unashauriwa kupunguza umwagiliaji kadri zao linavyokua.
    Wanashauriwa wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna uache kumwagilia maji
    Nivizuri kuthibiti magugu na kulimia kwakupandishia udongo ili vitunguu visiungue na jua.Katika hili epuka kutifulia kwa kina ili usikate mizizi ya vitunguu.

    Wengi wanasema zoezi zima la kupanda mpaka kuvuna vitunguu linakuwa kati ya siku 90 mpaka siku 150 ila hii inategemeana na aina za mbegu.

    CHANGAMOTO ZA MAGONJWA

    Zipo changamoto za magonjwa na wadudu wanaoweza kukwamisha au kupunguza uzalishaji wa zao hili,changamoto hizo ni kama :
    • Viroboto wa vitunguu,
    • Ukungu mweupe
    • Ukungu wa kahawia
    • Ugonjwa wa kuoza mizizi

    Ni vyema kuwasiliana na wataalamu wa kilimo kabla ya kuanza kilimo hichi ili kuweza kupata kinga au angalizo ya nini kufanya kutatua changamoto hizi.

    UVUNAJI WA VITUNGUU

    Utagundua kuwa vitunguu viko tayari kuvunwa baada ya kuona kuwa karibu asilimia 50 au nusu ya mimea shambani inaanza kuanguka na majani kukauka. Uvunaji ufanyike kwa kung’oa baada ya kumwagilia maji bustani siku moja kabla ya kuvuna.

    Baada ya kuvuna kata majani kama sentimeta 2 juu ya tunguu (usikate chini sana ya shingo wala kitako cha kitunguu kwani hii husababisha kuoza kwenye ghala au gunia la kusafirishia na kuenea kwa magonjwa. Baada ya hapo kitunguu kianikwe juani kwa siku 1 hadi 2.

    SOKO LA VITUNGUU

    Kutokana na uhitaji wa matumizi ya kila siku ya zao hili la vitunguu,uhitaji wake umekuwa mkubwa siku kwa siku.Wapo watu walioweza ona fursa hii na kuamua kuifanyia kazi.

    Kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa inchini kwetu,ni vyema tukaweza jua bei yake ili kumwezesha mtu kutambua uhalisia wake.

    Be ya kuuzia vitunguu shambani wakati was msimu wa vitunguu na endapo vimelimwa kwa wingi basi bei ya gunia inakuwa kati ya shilingi za kitanzania 60,000/= mpaka 80000/=.

    Inapokuwa sio wakati wa msimu na walimaji wamekuwa wachache na sokoni uhitaji unakuwa ni mkubwa basi bei yake ni kati ya shilling za kitanzania 150,000/= mpaka 200,000/=

    Bei za sadolini kwa sehemu zilizombali na soko ni kati ya shilingi za kitanzania 7,500/= mpaka 8,000/=

    Bei ya kilo moja kwa sehemu zilizombali na soko ni kati ya shilingi 2800/= mpaka 3500/=

    Zao hili linafaida kuanzia shambani mpaka mtumiaji wa mwisho.Ni vyema kabla ya kuanza kilimo hichi kuhakikisha umetatua maswala yafuatayo:
    • Eneo(kununua au kukodi),
    • Maji(kilimo cha umwagiliaji au kutegema mvua),
    • Nguvu kazi kwa ajili ya maandalizi ya shamba
    Msimamizi(Kujua kama utasimamia wewe mwenyewe au utamwajiri mtu kwa kazi hiyo)
    Gharama(gharama za maandalizi,upandaji,ukuzaji,uvunaji na utafutaji wa masoko na uuzaji)

    Tunaimani ukizingatia haya itakusaidia kujua uanze na mradi wa ukubwa gani.Fursatz.com inaimani kwa maelezo haya machche itakusaidia kupata mwanga zaidi juu ya fursa hii na endapo utaitaji kuuanza utajua ni wapi pa kuelekea ili kupata maelezo sahihi ya kiutaalamu.

    Kama kuanya maamuzi ndio moja kati ya sifa ambazo mjasiriamali inabidi awe nazo basi zitasaidia kukuwezesha kufanya maamuzi au kumsaidia ndugu,jamaa au rafiki kufanya maamuzi ya kweli kutoka katika hali aliyonayo sasa.

    No comments:

    Post a Comment

    Fashion

    Beauty

    Travel